View Full Version : Swahili Speaking Forum | Jukwaa La Kiswahili

Kwame
August 1st, 2009, 09:37 PM
I want to learn Swahili as soon as I finish with learning Portuguese, so I made this thread for all of you Swahili speakers out there. I think that this thread will attract more forumers considering Swahili is used heavily by East African internet users. Please limit the use of English in here, the only reason I'm using it is because I'm completely illiterate when it comes to this beautiful language. Also, sorry about the title, I tried my best.

Penye nia pana njia. :)

ernestombayo7
August 2nd, 2009, 06:52 AM

Sawa.Asante kwa kufikiria jambo la busara kama hii.Lakini wakenya wengi wana shida kuandika kiswahili.

desert burner
August 2nd, 2009, 10:02 AM
^^ ninafuraha chungu nzima kuona ndugu yetu amejitahidi kujua lugha ya kiswahili. karibu sana bwana kwame:banana:

BUTEMBO21
August 2nd, 2009, 10:17 AM
Lakini wakenya wengi wana shida kuandika kiswahili.

Ile ni bupumbafu, bana shindwa ku andika luga yabo.:ohno:

ernestombayo7
August 2nd, 2009, 04:11 PM
Ile ni bupumbafu, bana shindwa ku andika luga yabo.:ohno:

Wakenya kutoka Nairobi na miji kubwa kenya wanaongea Sheng.Yenye ni Kiswahili imechanganyishwa na Kiingereza.(spelling!?). Kwa hivyo hawajui Swahili sanifu.Hata mimi na ng'ang'ana sana.

Kenguy
August 2nd, 2009, 04:40 PM
I want to learn Swahili as soon as I finish with learning Portuguese, so I made this thread for all of you Swahili speakers out there. I think that this thread will attract more forumers considering Swahili is used heavily by East African internet users. Please limit the use of English in here, the only reason I'm using it is because I'm completely illiterate when it comes to this beautiful language. Also, sorry about the title, I tried my best.

Penye nia pana njia. :)

^^
Congrats. You got the Swahili proverb (Methali) right.:)

Kenguy
August 2nd, 2009, 04:41 PM
Wakenya kutoka Nairobi na miji kubwa kenya wanaongea Sheng.Yenye ni Kiswahili imechanganyishwa na Kiingereza.(spelling!?). Kwa hivyo hawajui Swahili sanifu.Hata mimi na ng'ang'ana sana.

Tunaweza kutumia 'sheng' hapa?:lol:

...ama wacha tuandike swahili sanifu tuone kama tunakumbuka kile tulichofanya shuleni. Hatukufunzwa lugha hii miaka karibu 12 bure. Kazi ngumu kuandika kwa Kiswahili.

ernestombayo7
August 2nd, 2009, 08:05 PM
Tunaweza kutumia 'sheng' hapa?:lol:

...ama wacha tuandike swahili sanifu tuone kama tunakumbuka kile tulichofanya shuleni. Hatukufunzwa lugha hii miaka karibu 12 bure. Kazi ngumu kuandika kwa Kiswahili.

Kweli kabisa.Wacha tujikakamue.Umewahi kujaribu kuzungumza na wa Tanzania?nakuambia maneno zinaweza kukupita kama gari ya safari rally.
Sijaandika na kiswahili kwa muda mrefu mpaka naskia ni kama naandika French.

BUTEMBO21
August 3rd, 2009, 01:34 AM
Wakenya kutoka Nairobi na miji kubwa kenya wanaongea Sheng.Yenye ni Kiswahili imechanganyishwa na Kiingereza.(spelling!?). Kwa hivyo hawajui Swahili sanifu.Hata mimi na ng'ang'ana sana.

Ata BaKongomani bana semaka Kifransa, alakini banajuwa Kuandika Swahili ya Kongo.

BUTEMBO21
August 3rd, 2009, 01:36 AM
Tunaweza kutumia 'sheng' hapa?:lol:

...ama wacha tuandike swahili sanifu tuone kama tunakumbuka kile tulichofanya shuleni. Hatukufunzwa lugha hii miaka karibu 12 bure. Kazi ngumu kuandika kwa Kiswahili.

Swahili sanifu? njo ya wapi ?

ewangai
August 3rd, 2009, 10:44 AM
Kiswahili kilizaliwa zanzibar, kikaendeleshwa Tanganyika, kikapatwa na ugonjwa kenya, kikafa uganda na mwishowe kikazikwa Congo.

Ni vizuri kujua kwamba ndugu yetu Mghana angependa kuongea Kiswahili. Ndio nasi tumsaidie na tujisaidie pia kwa kumfunza na kujikumbusha kiswahili.

Basi kwam nitaanza (I start)

Basic

Q. Hujambo (Hello, how are you)
R. Sijambo (I am well)

Q. Habari (Literal "News?" in an inquisitive manner used as salutation in a "how are things" manner)
R. Njuri / Njema / (Good, Fine)

Habari za Asubuhi (Morning) Mchana (Daytime) Jioni (evening)

Q. Vargrants, like most of us from nairobi, will probably just say
"Sema" which is fairly rude in say tanzania (Literal Say something)
R. Poa (Literal & Meaning "Cool" as you would use it in english)

come on lads, expand this

ewangai
August 3rd, 2009, 10:46 AM
Butembo your swahili reads like an indian accent. almost made me fall off my chair

kenyan24
August 3rd, 2009, 10:51 AM
Ya, that congo swahili is funny.

kenyan24
August 3rd, 2009, 10:56 AM
Nilipokuwa kidato cha kwanza nilikuwa sikipendi kiswahili hata tone. Lakini baada ya mda hayo yalibadilika, na nilipita kiswahili vizuri. Ladba sababu moja ni kwa sababu nina mizizi kutoka mkoa wa pwani. Ingekuwa vyema kama wakenya wangejikakamua kuongea kiswahili sanifu kama wafanyavyo watanzania.

Kenguy
August 3rd, 2009, 11:14 AM
Ya, that congo swahili is funny.

Ningependa kila mtu andike kile anachokijua kwa kiswahili. Watu wanaoishi nchi tofauti wanaandika na wanatamka Kiswahili kwa njia tofauti. Kwa mfano mtu anayetoka Kenya akisema "unaenda wapi" mwenzake kutoka Uganda atasema "onaenda wapi". Bora sisi sote tunaelewana. Pia ningetaka kujua namna Kiswahili cha Kongo kinachoandikwa. Labda Butembo anaweza kutusaidia.

desert burner
August 3rd, 2009, 07:18 PM
Butembo your swahili reads like an indian accent. almost made me fall off my chair

^^damn ewangai, i saw it i was laughing until my ribs were out but i could not say anything since he is a good friend of mine:lol:

kiswahili nilikuwa nikichukia sana wakati nilikuwa kidato cha kwanza kwa vile huko mkoa wa kaskazini mashariki tunatumia kisomali sana na pia huyo mwalimu alikuwa akinionea sana kwa hivyo nilikuwa nikitoroka kipindi cha kiswahili kabla mwalimu hakuhudhuria darasani na kujificha msalani:lol::lol:

BUTEMBO21
August 3rd, 2009, 09:02 PM
Butembo your swahili reads like an indian accent. almost made me fall off my chair

Indian accent? damn, .... Apana mwanaume, Njo Swahili ya kweli.:lol: Nyiye muko na "Swahili ya pembeni ya mayi". ( Coast Swahili.)
Yetu ni "Swahili ya Ndani " (Inland Swahili)

Alakini mi' napendaka basichana ya Kenya na Tanzania vile banasemaka Swahili.:cheers:

ewangai
August 5th, 2009, 01:12 PM
Lol

Zaitwa Lahaja. Nyie mwaongea lahaza ya Kingwana, Sisi wanairobi twaongea sheng ama Kimvita (Mombasa) au Kiamu (Lamu)

Kuna orodha ya lahaja mbali mbali kwenye kamusi elezi ya wikipedia

* Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.
* Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
* Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
* Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
* Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.
* Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
* Kingwana: Kiswahili cha Kongo
* Shikomor: Kiswahili cha Komoro
* Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
* Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
* Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
* Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba
* Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia
* Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya

ernestombayo7
August 5th, 2009, 01:48 PM

Safi!

Kenguy
August 6th, 2009, 11:12 PM
Sikujua sheng ni lahaja ya Kiswahili.

Papaf Mwenyewe
August 7th, 2009, 06:28 PM
Know Your AFRICAN Founding Fathers (In a Swahili Tongue Twister)

NYERERE KAUNDA BANDA AZIKIWE KENYATTA

Kenguy
August 8th, 2009, 05:36 AM
Know Your AFRICAN Founding Fathers (In a Swahili Tongue Twister)

NYERERE KAUNDA BANDA AZIKIWE KENYATTA

^^
Sasa wewe, uliipata wapi? Ama ulikaa chini na kufikiria kuunganisha majina kutunga sentensi? :lol: Heko ndugu!

Papaf Mwenyewe
August 8th, 2009, 07:58 AM
Kwa Lahaja, msisahau

KIJOMVU

KICHANGAMWE

Kenguy
August 12th, 2009, 07:39 PM
Nimerudi kutoka safari nchini Tanzania na kuna kitu kimoja nimegundua. Sisi Wakenya hatujui Swahili. Kweli Wabongo wanaipenda lugha.

Kama jana niliingia duka ili niweze kutuma barua pepe katika mtandao nilikuta wanatumia Google katika lugha ya Kiswahili. Kuhesabu pesa kwa Kiswahili kwangu ilikuwa ngumu kwa sababu walikuwa wananiambia bei ya bidhaa kwa Kiswahili halafu nilijikuta nikifikiria bei kwa kiingereza kabla ya kununua kitu chochote. Habari za saa tatu Tanzania wanasoma kutumia Kiswahili wakati mimi nimezoea kusikia Habari za Kiingereza saa hizo nikiwa nyumbani Kenya. Kile kilichonifurahisha sana ni vile Watanzania wanachukua kila mtu kuwa kama ndugu wao. Mtu akiniita na hanijui Uganda anasema gwe, Kenya ni wewe lakini Tanzania ni Ndugu... Nilifurahi sana!

Dar es salaam imeendelea sana. Si kama vile nilikuwa nimefikiria hapo mbeleni. Nitaziweka picha zile nilichukua katika uzi {if thats what you call a thread in Swahili} ya Dar es salaam nikipata wakati.

TZ, Hongera.

kenyan24
August 12th, 2009, 07:57 PM
Ati uzi?? Hehehe. Mimi nimetembelea site za watanzania katika mtandao na kwa kweli nimeshuhudia chuki kubwa sana dhidi ya wakenya. Hata sasa sina hamu ya kwenda kule. Je ulishuhudia chuki hii? Marafiki zangu waniambia kule hawarudi, kila waendako wanaitwa mungiki.

Kenguy
August 13th, 2009, 04:45 AM
Ati uzi?? Hehehe. Mimi nimetembelea site za watanzania katika mtandao na kwa kweli nimeshuhudia chuki kubwa sana dhidi ya wakenya. Hata sasa sina hamu ya kwenda kule. Je ulishuhudia chuki hii? Marafiki zangu waniambia kule hawarudi, kila waendako wanaitwa mungiki.

Nilikuwa huko kama siku nne tu. Na wakati huo wote sikumpata mtu hata mmoja aliyenionesha madharau au chuki. Labda wako lakini sikuwakuta. Huwezi sema watu ni wabaya kwa sababu ya kile wanachoandika katika mtandao. Ukisema hivo, basi Wakenya ndio wabaya zaidi (angalia mashada kwa mfano). Na wale wanaotumia mtandao wengi wako nchi za ulaya sio Tanzania. Kila nchi iko na watu wenye roho mbaya na wale wazuri.

KQV208
August 13th, 2009, 07:02 AM
Habari nyote? Kiswahili changu si kizuri vile. Nimesahau kidogo kwani sikukifuatilia baada ya kuondoka kidato cha mwisho. Lakini sasa tutakirekebisha hapa hapa. Siku njema.

BUTEMBO21
August 13th, 2009, 09:38 AM
Nilikuwa huko kama siku nne tu. Na wakati huo wote sikumpata mtu hata mmoja aliyenionesha madharau au chuki. Labda wako lakini sikuwakuta. Huwezi sema watu ni wabaya kwa sababu ya kile wanachoandika katika mtandao. Ukisema hivo, basi Wakenya ndio wabaya zaidi (angalia mashada kwa mfano). Na wale wanaotumia mtandao wengi wako nchi za ulaya sio Tanzania. Kila nchi iko na watu wenye roho mbaya na wale wazuri.

Chali, Ni patiye ile site ya baTanzania, ni ba chambule ko kidogo. Tafazali.

kenyan24
August 13th, 2009, 11:42 AM
Yaitwa jamiiforums.com

BUTEMBO21
August 13th, 2009, 05:58 PM
Yaitwa jamiiforums.com

Aksante ,

But damn, aba baTZ nini iko mukichwa yabo?:ohno:

kenyan24
August 13th, 2009, 06:08 PM
Haha, kwanini wauliza hivyo?

BUTEMBO21
August 13th, 2009, 06:12 PM
Haha, kwanini wauliza hivyo?

Ba TZ mingi abapendi Kenya, ama EAC, bana ogopa Kenya sana.

kenyan24
August 13th, 2009, 08:30 PM
Kweli kabisa, there was a study a while back iliyosema over 70% of watanzania hawataki EAC.

BUTEMBO21
August 14th, 2009, 02:07 AM
Kidogo ya Swahili ya Kongo.

Month = Mwezi.

January = Mwezi ya Kwanza
Feb = Mwezi ya Pili
Mar = Mwzi Ya Tatu
Apr =........ ya Ine
May =......... ya Tano
June =..........ya Sita
Jul =.........ya Saba
Aug =..........Ya Mnane
Sept =.........ya Kenda
Oct =,.........ya Kumi
Nov =.........ya Kumi na Moya
Dec =.........ya kumi na Mbili

Week = Juma.
dAY =Siku.

Monday = Siku ya Kwanza
Tues = ......ya Pili
Wedn =.......ya Tatu
Thusd =........ya Ine
Fri =........ya tano
Sut =.......ya Sita
Sun = Siku Ya Mungu.

Zero = Sero
One = Moya
Two = Mbili
Three = Tatu
Four = Ine
Five = Tano
Six = Sita
Seven =Saba
Eight =Munane or Mnane
Nine =Kenda
Ten = Kumi
Eleven = Kumi Namoya
Nineteen = Kumi na Kenda

20= Makumi mbili
21= Makumi mbili na moya

29=Makumi mbili na kenda
30=Makumi tatu

50=Makumi tano
60=Makumi sita
70=Makumi saba
80=Makumi munane or Mnane
90= Makumu Kenda

100 Mia Moya/Mia Moja ( depends)
1000 Elfu Moya/Moja. ( depends)

Father= Baba
Mother=Mama
Sister= Dada
Brother= kaka
Grandma= Tate Mwanamuke or (Nkambo for Katangan Swahili)
Grandpa= Tate Mwana ume or (Nkambo for Katangan Swahili)
Uncle= Muyomba
Aunt= Shangazi

Mwafrika
August 14th, 2009, 11:52 PM
^^ wa congo mna piga hesabu kwa namna ya ku shangaza:)
(I mean to say the way you count is interesting)

Ishirini (20) mna sema makumi mbili
thelathini (30) makumi tatu... na kadhalika
arubaini - 40
hamsini - 50
sitini - 60
sabini - 70
themanini - 80
tisini - 90
mia - 100

BUTEMBO21
August 15th, 2009, 01:10 AM
^^ wa congo mna piga hesabu kwa namna ya ku shangaza:)
(I mean to say the way you count is interesting)

Ishirini (20) mna sema makumi mbili
thelathini (30) makumi tatu... na kadhalika
arubaini - 40
hamsini - 50
sitini - 60
sabini - 70
themanini - 80
tisini - 90
mia - 100

Woooooow , Si wezi ku esabia vile mweye muna esabia.:rofl:

Kwame
August 22nd, 2009, 01:43 AM
Sawa.Asante kwa kufikiria jambo la busara kama hii.Lakini wakenya wengi wana shida kuandika kiswahili.

^^ ninafuraha chungu nzima kuona ndugu yetu amejitahidi kujua lugha ya kiswahili. karibu sana bwana kwame:banana:

Translation? :D

^^
Congrats. You got the Swahili proverb (Methali) right.:)

Thanks bro, what would have been the Kiswahili equivalent of writing Kiswahili speaking forum?

BUTEMBO21
August 22nd, 2009, 03:00 AM
Translation? :D

Thanks bro, what would have been the Kiswahili equivalent of writing Kiswahili speaking forum?

Congolese Swahili is easy, Kenya/ Tanzania Swahili is damn too hard.

Kisumu Ndogo
August 22nd, 2009, 03:01 AM
Translation? :D

Thanks bro, what would have been the Kiswahili equivalent of writing Kiswahili speaking forum?

I will try to help I think there are several ways you can put it, Example

Translation
Zimo njia nyingi ambazo waweza kusema msemo huo. Mfano

Ukumbi wa gumzo ya Kiswahili
Mdahalo wa lugha ya Kiswahili^^

Kenguy
August 22nd, 2009, 12:40 PM
Congolese Swahili is easy, Kenya/ Tanzania Swahili is damn too hard.

Usife moyo.:) Kiswahili yetu si ngumu.

BUTEMBO21
August 22nd, 2009, 07:16 PM
Usife moyo.:) Kiswahili yetu si ngumu.

Apana mwanaume, ile Swahili yenu iko nguvu sana.

Kwame
September 15th, 2009, 12:28 AM
I will try to help I think there are several ways you can put it, Example

Translation
Zimo njia nyingi ambazo waweza kusema msemo huo. Mfano

Ukumbi wa gumzo ya Kiswahili
Mdahalo wa lugha ya Kiswahili^^

Ahsante. :)

Kenguy
October 3rd, 2009, 09:40 PM
Dar es Salaam miaka 10 ijayo

Mwananchi,
10/2/09.
Sadick Mtulya.

PAMOJA na majiji mbalimbali duniani kuwa ya kuvutia kutokana na kujengwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, yanahitaji kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara ili kuyafanya yaende na wakati na kuzidi kuwa ya kisasa wakati wote.

Kama ilivyo kwa mengine, Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji yaliyo na jiografia nzuri na ya kipekee. Hiyo inatokana na kuwa na sehemu kubwa ya ardhi yenye uoto wa asili ambao kama utaboreshwa kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za makazi bora, litakuwa moja ya majiji bora kati ya machache Afrika.

Kumekuwa na jitihada za kuliboresha jiji la Dar es Salaam na moja ya mradi mkubwa uliopendekezwa katika miezi ya karibuni ni ule utakaogharimu zaidi ya Sh1.4 trilioni. Rasimu ya mradi huo ilishazinduliwa na Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT), Afrika na Uarabuni Dk Aliounce Badiane.

Dk Aliounce Badiane anasema mradi huo unaanza kwa kiwango cha Sh800 bilioni na tayari mkakati wa kudhibiti maeneo ambayo hayajajengwa umekwishaanza.

Mradi huo umezingatia maeneo makuu matatu ambayo ni ugawaji na upangaji bora wa ardhi, huduma za jamii pamoja na ujenzi wa makazi bora yatakayoendana na uwezo na uhalisia wa maeneo husika.

Mradi wa kulikarabati jiji hilo utakuwa wa miaka 10 kuanzia 2010 mpaka 2020 ikiwa ni sehemu ya mpango wa UN-HABITAT kuboresha makazi duni ya majiji mbalimbali barani Afrika.

Jiji la Dar es Salaam limepata nafasi hiyo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu ya zaidi ya milioni tatu ambalo ni ongezeko la watu 100,000 sawa na asilimia 4.3 kila mwaka. Inakadiriwa kwamba hadi mwaka 2015 litakuwa na watu zaidi ya milioni 3.8

Uboreshaji huo utalifanya kuwa moja kati ya majiji makubwa yaliyopangika kwa kufuata utaratibu wa sera na sheria za makazi duniani.

Ofisa Mwandamizi wa jiji la Dar es Salaam anasema mradi huo umekuja katika muda muafaka hasa ikizingatiwa kwamba asilimia 70 ya maeneo ya Dar es Salaam yamejengwa kiholela.

Anasema: “Huu mradi ni mkubwa na unahitaji ushirikiano katika nyanja zote hivyo wananchi waupokee na watoe ushirikiano kwa wadau watakaofika katika maeneo yao kwa ajili ya shughuli mbalimbali.”

Katika mradi huo, uboreshaji utakuwa katika awamu tatu zinazokwenda sambamba. Katika kila eneo kuna mipango mitatu ambayo ni ya muda mfupi (Julai 2009 - Juni 2010), muda wa kati (2010 - 2015) na muda mrefu (2016- 2020).

Suala la Ardhi
Mikakati ya muda mfupi iliyoanza Julai 2009 hadi Juni 2010 itakuwa ni ya uboreshaji wa uoto wa asili.

Muda wa kati, utakaoanzia 2010 hadi 2015 utakuwa ni kuainisha kwa uwekaji wa maeneo ya wazi, upitaji wa barabara, pamoja na kuonyesha maeneo yanayofaa kuwepo huduma mbalimbali za kijamii.

Muda mrefu, utakayoanza 2016/20 utahusisha ugawaji wa viwanja 150,000 vilivyopimwa katika Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni, kutoa hatimiliki pamoja kuongeza ongezeko la ulipaji kodi kutoka asilimia 20 hadi 40.

Huduma za jamii

Mikakati ya muda mfupi iliyoanza Julai 2009 hadi Juni 2010 inahusisha ujenzi wa vyoo vikubwa vitatu vya jamii, ujenzi wa mtandao mkubwa wa upatikanaji wa maji safi pamoja na utoaji majitaka.

Muda wa kati, utakaoanza 2010 hadi 2015, utahusisha ujenzi wa miondombinu ya barabara yenye mifereji zinazotoka nje ya mji zenye urefu wa kilomita 54 na za ndani ya jiji kwa kilomita 20, ujenzi wa vituo 90 vya kutoa huduma ya majisafi na salama, ujenzi wa vyoo 159 pamoja na kujenga mfumo imara wa mifereji ya majitaka.

Muda mrefu, kuanzia 2016 - 2020 utahusisha ujenzi wa shule 10, zahanati 20, masoko 20, kuiwezesha Dawasa kutoa huduma ya utoaji majitaka kutoka asilimia 10 hadi 30, pamoja na ujenzi wa maeneo ya kuhifadhi majitaka.

Ujenzi wa nyumba

Mikakati ya muda mfupi, iliyoanzia Julai 2009 hadi Juni 2010 ikihusisha kuwajengea uwezo na kuwapa utaalamu zaidi mafundi ujenzi pamoja na kuwawezesha wananchi hususan katika ujenzi wa nyumba bora.

Muda wa kati, kuanzia 2010 - 2015 utahusisha uboreshaji na upatikanaji wa vifaa vya ujenzi vilivyo bora na kwa bei nafuu, uboreshaji wa ulipaji fidia, mkopo wa nyumba kwa bei nafuu pamoja na kuwajengea uwezo wenyeviti wa mitaa kwa kuanzisha sheria ndogondogo.

Muda mrefu, itakayoanzia 2016 mpaka 2020 itahusisha ujenzi wa nyumba binafsi za kupangisha, uimarishaji wa namba za nyumba pamoja na kuwajengea uwezo wakazi wenye maisha duni kuendelea kuishi katika nyumba za mijini na si kukimbilia nje ya mji na kujenga nyumba kiholela.

Pamoja na mikakati hiyo baadhi ya wadau wanataka mradi huo kuangalia kwa umakini uwepo wa kambi za jeshi, vituo vya mafuta pamoja na vitu vinavyoweza kusababisha milipuko katika makazi ya watu.

Fedha za kufanikisha mradi zitachangiwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali kuu, Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, nchi wahisani, Un-Habitat, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, pamoja na watu binafsi.

Mradi kama huo umekwishafanyika katika nchi nyingi duniani ikiwemo Istanbul, Uturuki uliofanywa mwaka 1960 na mwaka 1995 katika baadhi ya majiji ya Afrika Kusini.

Miji mingine ya Afrika iliyo katika mpango huo ni ya mataifa ya Chad na Burkina Faso.

Tuma maoni kwa Mhariri.

BUTEMBO21
October 3rd, 2009, 11:13 PM
^^ damn Kenguy, this thing is too hard, it took me 3 minutes to read and only understood 30% of it.:ohno:

Kenguy
October 4th, 2009, 05:06 AM
^^ damn Kenguy, this thing is too hard, it took me 3 minutes to read and only understood 30% of it.:ohno:

Butembo, can you do me a favour and post an article in Congolese swahili? Then maybe we can compare notes.

Kwame
October 16th, 2009, 08:15 AM
Since no one has anything to say, does anyone want to go over the basics of Kiswahili (alphabet, pronunciations, different dialects, etc)??

funkydory
October 16th, 2009, 02:16 PM
Since no one has anything to say, does anyone want to go over the basics of Kiswahili (alphabet, pronunciations, different dialects, etc)??

It will help me too. I'm a mzungu who works for an African NGO here in England. Don't be shy of including any rude words whatsoever. i want to impress my work colleagues here and be the life and soul of the next garden party i get invited to (2 so far) at the Kenyan High Commissioner's private residence in London:lol::banana:

Kenguy
October 16th, 2009, 09:04 PM
Since no one has anything to say, does anyone want to go over the basics of Kiswahili (alphabet, pronunciations, different dialects, etc)??

The alphabet is the same as the normal one only that there is no letter Q in Swahili. Also all words are built around the vowels A, E, I, O, U (all words also end with a vowel as well.) The vowels are the most dominant sounds when pronouncing swahili words.

Example:

Mama (mother)- mAmA
Habari yako (how are you)-hAbArI yAkO

Damn... I guess I'd make a lousy teacher.

Kenguy
October 16th, 2009, 09:13 PM
It will help me too. I'm a mzungu who works for an African NGO here in England. Don't be shy of including any rude words whatsoever. i want to impress my work colleagues here and be the life and soul of the next garden party i get invited to (2 so far) at the Kenyan High Commissioner's private residence in London:lol::banana:

Maybe you can post words, sentences or phrases you want to know which we can then translate and help with the pronounciation.:)

BUTEMBO21
October 19th, 2009, 08:05 AM
Korth , South Kivu Kiswahili.

jXieh2Z0uX0&feature

desert burner
October 19th, 2009, 08:18 AM
^^aha, sema hivyo na mbona nime fahamu yote maneneo ya hawa waimbaji:) lakini wewe ukiandika basi sijui hakuna tofauti na mhindi:lol::lol:

BUTEMBO21
October 19th, 2009, 08:37 AM
^^aha, sema hivyo na mbona nime fahamu yote maneneo ya hawa waimbaji:) lakini wewe ukiandika basi sijui hakuna tofauti na mhindi:lol::lol:

Muhindi?lol. ngoya mita kuonesha vile bahindi banasemaka.

Kuandika yetu iko tafaouti kidogo naya Kenya na TZ.

BUTEMBO21
October 19th, 2009, 08:49 AM
Kiswahili ya mu Katanga.

foward at 1:34

X2Etq7vrDhs

Kwame
October 27th, 2009, 01:32 AM
The alphabet is the same as the normal one only that there is no letter Q in Swahili. Also all words are built around the vowels A, E, I, O, U (all words also end with a vowel as well.) The vowels are the most dominant sounds when pronouncing swahili words.

Example:

Mama (mother)- mAmA
Habari yako (how are you)-hAbArI yAkO

Damn... I guess I'd make a lousy teacher.

Thanks man. Don't be so hard on yourself, this stuff is really going to help me once I enroll in a Kiswahili language course. :)

Kwame
October 27th, 2009, 01:34 AM
A few days ago I found this conscious rap song in Kiswahili that I really like.

CFfxfUXmSG4

The subtitles say he's talking about the struggles the poor go through on a daily basis in Tanzania.

Kenguy
October 27th, 2009, 11:20 PM
A few days ago I found this conscious rap song in Kiswahili that I really like.

CFfxfUXmSG4

The subtitles say he's talking about the struggles the poor go through on a daily basis in Tanzania.

I have problems viewing videos at the moment. Guess I will wait until I get to a location with a better connection.

Kenguy
October 27th, 2009, 11:35 PM
Greetings:

The most common; Habari yako (how are you) reply (mzuri) Im fine.

Shikamoo (Hello) Reply: Marahaba. Shikamoo is used when greeting an older individual, especially in Tanzania and the Kenyan coast.

Sabalkheri (Good Morning)

Masalkheri (Good Evening)

Habari za asubuhi (Good morning)

Habari za jioni (Good evening)

Habari za mchana (Good afternoon)

Salaam aleikum (peace be upon you) Reply: Aleikum salaam (peace be upon you too).

Sema. (Hello) Reply: Poa (fine, no problem) Commonly used in most urban areas in Kenya and Tanzania, sort of like slang.

BUTEMBO21
November 2nd, 2009, 04:43 PM
Katanga's Swahili.

Nyota TV's Swahili Bora. Kenguy, i'm late , we now have Swahili Bora.
idCnvoA40EI

The same TV has the version of the Swahili Facila( Easy Swahili that is spoken around the city and Katanga).

DP0sK82ogjY

ombithu
November 19th, 2009, 09:28 AM
Mimi ni mkenya hapa malaysia anayekienzi sana kiswahili. Nilipokuja kuja hapa nilishangazwa sana na jinsi kiswahili kilivyoenea. Nina marafiki warabu kutoka dubai na saudi arabia ambao hawajahi toka nchi zao kwenda afrika mashariki lakini wanazungumza kiswahili fasaha kabisa (kiunguja) hata ilinibidi niwaitishe paspoti zao kuhakikisha hawajafika afrika mashariki. Waafrika wengine nao kama wazimbabwe na wabotswana hupenda kutuambia tuwatafsirie maneno yote kwa kiswahili, wao hutamani sana kuongea kiswahili. Itakuwa ni vibaya na aibu sana kwetu wakenya kukipuuza kiswahili kwani kuna watu wengine ambao wanatamani hiyo ndiyo ingekuwea lugha yao. Hata hawa wamalaysia wenyewe husema lugha yetu inavutia.

Kenguy
November 19th, 2009, 09:53 PM

Mkenya wa pili kutoka Malaysia hapa SSC. Karibu.:)

Kenguy
November 19th, 2009, 09:56 PM
Katanga's Swahili.

Nyota TV's Swahili Bora. Kenguy, i'm late , we now have Swahili Bora.
idCnvoA40EI

The same TV has the version of the Swahili Facila( Easy Swahili that is spoken around the city and Katanga).

DP0sK82ogjY

Is Nyota TV a nationwide station or is it just broadcast in Katanga?

Kenguy
November 26th, 2009, 09:30 PM
Found a short article.

It is an undeniable truth that Arab and Persian cultures had the greatest influence on the Swahili culture and the Swahili language. To demonstrate the contribution of each culture into the Swahili language, take an example of the numbers as they are spoken in Swahili. "moja" = one, "mbili" = two, "tatu" = three, "nne" = four, "tano" = five, "nane" = eight, "kumi" = ten, are all of Bantu origin. On the other hand there is "sita" = six, "saba" = seven and "tisa" = nine, that are borrowed from Arabic. The Arabic word "tisa" actually replaced the Bantu word "kenda" for "nine". In some cases the word "kenda" is still used. The Swahili words, "chai" = tea, "achari" = pickle, "serikali" = government, "diwani" = councillor, "sheha" = village councillor, are some of the words borrowed from Persian bearing testimony to the older connections with Persian merchants.

The Swahili language also absorbed words from the Portuguese who controlled the Swahili coastal towns (c. 1500-1700AD). Some of the words that the Swahili language absorbed from the Portuguese include "leso" (handkerchief), "meza" (table), "gereza" (prison), "pesa" ('peso', money), etc. Swahili bull-fighting, still popular on the Pemba island, is also a Portuguese legacy from that period. The Swahili language also borrowed some words from languages of the later colonial powers on the East African coast - English (British) and German. Swahilized English words include "baiskeli" (bicycle), "basi" (bus), "penseli" (pencil), "mashine" (machine), "koti" (coat), etc. The Swahilized German words include "shule" for school and "hela" for a German coin.

Hassan O. Ali

BUTEMBO21
November 27th, 2009, 12:32 AM
Found a short article.

It is an undeniable truth that Arab and Persian cultures had the greatest influence on the Swahili culture and the Swahili language. To demonstrate the contribution of each culture into the Swahili language, take an example of the numbers as they are spoken in Swahili. "moja" = one, "mbili" = two, "tatu" = three, "nne" = four, "tano" = five, "nane" = eight, "kumi" = ten, are all of Bantu origin. On the other hand there is "sita" = six, "saba" = seven and "tisa" = nine, that are borrowed from Arabic.

MOJA in Coast Swahili and MOYA in Congolese Swahili.

NNE=4; Coest Swahili.

In Congo it's INE=4.

Arabic word "tisa" actually replaced the Bantu word "kenda" for "nine". In some cases the word "kenda" is still used.

Why did you guys change from Bantu ???????:bash:

The Swahili words, "chai" = tea, "achari" = pickle, "serikali" = government, "diwani" = councillor, "sheha" = village councillor, are some of the words borrowed from Persian bearing testimony to the older connections with Persian merchants.

SHAHA= Village councillor Cost Swahili.

MWAMI= Village Councillor in Congo.

The Swahili language also absorbed words from the Portuguese who controlled the Swahili coastal towns (c. 1500-1700AD). Some of the words that the Swahili language absorbed from the Portuguese include "leso" (handkerchief), "meza" (table), "gereza" (prison), "pesa" ('peso', money), etc. Swahili bull-fighting, still popular on the Pemba island, is also a Portuguese legacy from that period.

Lingala also borrowed from portugese MESA = is MESA.[Lingala].

PESA ;Is considered Tanzanian Swahili.[ according to the Kongolese].

But we use MAKUTA. and other Congolese use Franka or Franga [Borrowed from French for " FRANC".]

The Swahili language also borrowed some words from languages of the later colonial powers on the East African coast - English (British) and German. Swahilized English words include "]"baiskeli" (bicycle)[/SIZE], "basi" (bus), "penseli" (pencil), "mashine" (machine), "koti" (coat), etc. The Swahilized German words include "shule" for school and "hela" for a German coin.

SHULE? in Congo it's "MASOMO." and Now Congolese Swahili has borrowed from Lingala " CHIKI"= School.

HELA" ? Iin Congo it's "Kikoroto".

Baisikeli; ? In Congo it's "Kinga."

Kenguy
November 27th, 2009, 01:31 PM
MOJA in Coast Swahili and MOYA in Congolese Swahili.

Do you guys pronounce the Y in Moya or is the spelling just different? Most Congolese I have spoken to pronounce the J part as in MOJA, but maybe its because they are used to speaking the Kenyan version.

PESA ;Is considered Tanzanian Swahili.[ according to the Kongolese].
But we use MAKUTA. and other Congolese use Franka or Franga [Borrowed from French for " FRANC".]

The terms used for money vary from country to country in East Africa. In Kenya and Tanzania its Pesa, in Uganda its Ssente, in Rwanda its Kifaranga or faranga almost like you guys in the DRC.

Baisikeli; ? In Congo it's "Kinga."

Kinga in Kenyan swahili is take care.:lol:

Kenguy
November 27th, 2009, 02:13 PM
Swahili sentences can be combined in one word. Like other Bantu languages, the verb carries the subject or object connected by an affix that denotes the tense.

For example one can say niliongea to mean I had talked.

(Ni)-in this case denotes the subject (I/me) while Ongea means talk. Both the subject and the verb are connected by the affix, (li) which is used in reference to the tense which in this case is the past tense.

If it was in the present continuous tense, the sentence would be (Ninaongea) ie. I am talking.

The future tense would be nitaongea. (I will talk).

mwanamwiwa
November 27th, 2009, 02:13 PM
The terms used for money vary from country to country in East Africa. In Kenya and Tanzania its Pesa, in Uganda its Ssente, in Rwanda its Kifaranga or faranga almost like you guys in the DRC.

Kifaranga?Are they running barter trade or what!(joke).Kenguy,that was a nice article.Kenda must be a bantu name because in Kamba it means nine.

BUTEMBO21
November 27th, 2009, 08:27 PM
Do you guys pronounce the Y in Moya or is the spelling just different? Most Congolese I have spoken to pronounce the J part as in MOJA, but maybe its because they are used to speaking the Kenyan version.

Yes, Moja is usually pronounced when talking to Kenyans or TZns.

In Katanga, Oriental province , Maniema province, Moja doesn't even exist there.
It's mostly used in North and South Kivu provinces because our Swahili is closer to that of Kenya and TZns[ because of lots of Contacts and interactions with you guys.]

The terms used for money vary from country to country in East Africa. In Kenya and Tanzania its Pesa, in Uganda its Ssente, in Rwanda its Kifaranga or faranga almost like you guys in the DRC.

I know about the Ugandan term[ i like their term], In Rwanda Kifaranga/Faranga is borrowed from French [Franc] yeap very close to Congo's [ cause we both Use Francs].

Kinga in Kenyan swahili is take care.:lol:

:lol: interesting.

desert burner
November 29th, 2009, 07:46 AM
^^kinga or kujikinga is protection:) kwa mfano amenunua silaha iliajikinge maadui:lol: how about that:nuts: even though i have been away for sometime i think i am not that bad the fact that kiswahili was my worst subject in high school:)

BUTEMBO21
November 29th, 2009, 08:30 AM
^^kinga or kujikinga is protection:) kwa mfano amenunua silaha iliajikinge maadui:lol: how about that:nuts: even though i have been away for sometime i think i am not that bad the fact that kiswahili was my worst subject in high school:)

you actually good.

Kununua [ Kenya, TZ] = to buy

Kuuza [DRC] = To buy.

Kenguy
November 30th, 2009, 07:09 PM
you actually good.

Kununua [ Kenya, TZ] = to buy

Kuuza [DRC] = To buy.

Kuuza means to sell in Kenya.

BUTEMBO21
November 30th, 2009, 10:21 PM
Kuuza means to sell in Kenya.

We also use Kununua; but Kuuza is more common.

I used to be confused speaking to my Kenyans friends. about Kuuza and Kununua.

I remember my friends mom telling " Sasa?" i had no clue it was a greeting :lol:

I responded, " Sasa nini?":lol:

Kenguy
December 21st, 2009, 12:58 PM
Yes, Moja is usually pronounced when talking to Kenyans or TZns.

In Katanga, Oriental province , Maniema province, Moja doesn't even exist there.
It's mostly used in North and South Kivu provinces because our Swahili is closer to that of Kenya and TZns[ because of lots of Contacts and interactions with you guys.

^^
I met a Congolese guy 3 days ago in Western Uganda and he pronounced Moya with a strong Y emphasis instead of J. Glad you told me about it coz he was talking rather fast and I would have been slightly confused.

maasai1
December 23rd, 2009, 07:30 AM
We also use Kununua; but Kuuza is more common.

I used to be confused speaking to my Kenyans friends. about Kuuza and Kununua.

I remember my friends mom telling " Sasa?" i had no clue it was a greeting :lol:

I responded, " Sasa nini?":lol:
Ndugu Butembo, nashangaa vile wajua pia lugha ya kiingereza, kwa vile WaKongomani wengi hawaelewi Kiingereza. Ama umewahi ishi Kenya?:nuts:

BUTEMBO21
December 23rd, 2009, 09:17 AM
Ndugu Butembo, nashangaa vile wajua pia lugha ya kiingereza, kwa vile WaKongomani wengi hawaelewi Kiingereza. Ama umewahi ishi Kenya?:nuts:

Mina ishi Amerika njo mana.:lol:

BUTEMBO21
December 23rd, 2009, 09:20 AM
^^
I met a Congolese guy 3 days ago in Western Uganda and he pronounced Moya with a strong Y emphasis instead of J. Glad you told me about it coz he was talking rather fast and I would have been slightly confused.

Yea, Y is used in words like. Moya, Mayi, instead of Moja, Maji.

Kenguy
December 23rd, 2009, 10:21 AM
Yea, Y is used in words like. Moya, Mayi, instead of Moja, Maji.

^^
For a Kenyan, that can be really confusing. If a Congolese asked for water and said "nataka mayi" I can bet a Kenyan will look at you twice and try asking something like "Mayi? Mayai?...though eventually they will figure it out.

Lakini nilipenda vile huyo Mkongo alivyoongea Swahili. Ungetuona tukicheka tukiongea siasa za nchi zetu, ungefikiria sisi wawili ni marafiki tangu zamani.

maasai1
December 23rd, 2009, 11:17 AM
Mina ishi Amerika njo mana.:lol:

ok. I see, that expains something. Kenyans speak British english, which is more gentle, lacking words like 'damn' and others which would be taken to be unpallatable or rude in kenyan/british english.:lol: Americans love curse words like damn, bloody, f**k, s**t, etc.

maasai1
December 25th, 2009, 08:15 AM
More swahili words for Kwame:
Njoo- come, coastals pronounce it 'ndhoo'
enda- go
cheka- laugh
sema- say eg. sema kitu- say something
lala- sleep
kimbia- run
simama- stand up, or stop moving
penda- love, or like
nakupenda- I love you
simu- telephone
gari- motorvehicle
sijui- I don't know

more words to follow soon! kiswahili kidumu!

BUTEMBO21
December 25th, 2009, 08:25 PM
Lakini nilipenda vile huyo Mkongo alivyoongea Swahili. Ungetuona tukicheka tukiongea siasa za nchi zetu, ungefikiria sisi wawili ni marafiki tangu zamani.

Ile ni muzuri, niko na barafiki baKenya California, Rafikiyangu tangu miaka munane.

Mpaka leo siwezi andika kama BaKenya ao BaTanzania.

BUTEMBO21
December 25th, 2009, 08:27 PM
ok. I see, that expains something. Kenyans speak British english, which is more gentle, lacking words like 'damn' and others which would be taken to be unpallatable or rude in kenyan/british english.:lol: Americans love curse words like damn, bloody, f**k, s**t, etc.

Mie Napendaka vile Bangereza bana semaka Kingereza [ alakini Banamuke benyewe].:lol:

Fazla
February 9th, 2010, 04:50 PM
Salam Aleykum :D

I'm really interested in Swahili and have thought about starting to learn it... although unfortunately I don't have any plan to go to a Swahili speaking country in the foreseeable future. I'd like to know how exactly is Swahili spread in Kenya and Tanzania like... does everyone use it?? And in which other countries can you use Swahili? In which countries is it the most useful (this last question could be read as "Which country speaks English or French the least?)

And how good do people speak English or French? Especially educated people, I guess they all have a good command of these languages?

Because studying a language takes a lot of time and willingness and if there's something I'd hate, is having people who getting annoyed by my mistakes immediately switch to English/French...

Kisumu Ndogo
February 9th, 2010, 05:40 PM

Swahili(Origin corroboration of Arabic & Bantu languages) I believe is one of the easiest languages to learn atleast on the onset of it. In Tanzania-Zanzibar Swahili is very well spread throughout the country and thus spills overs to immediate borders of Mozambique, Zambia, Malawi, DRC, Comoro Is and even Angola(Cabinda). In Kenya Mombasa and Lamu Island speaks the 'sweetest swahili' (Lahaja -Mvita na Amu). In both Kenya and Tanzania its one of the Officially spoken languages alongside english. Although most of the Country communicates in swahili in Kenya, in Nairobi it is 'corrupted' by the entry of Sheng (Largely a mixture of Swahili -English, few French and mainly Bantu languages with few Nilotic words). As you move to the deeper hinterland of Kenya swahili is mixed with other ethnically spoken languages. Uganda also uses Swahili(Military and Politicians mainly) and so is Rwanda and Burundi.

Good thing since swahili is one of the most widely spoken languages in Africa alongside Arabic and Hausa excluding English and French it is taught in most bigger institutions of learning around the world, I would also suggest you try listen to broadcast like BBC Swahili service use Swahili|English dictionary(Kamusi) to look up words you do not understand, wish you best in the endeavor.

desert burner
February 11th, 2010, 11:43 AM
Mie Napendaka vile Bangereza bana semaka Kingereza [ alakini Banamuke benyewe].:lol:

let me try to rewrite what butembo wrote in kenyan version.

mimi napenda vile waengereza wana sema (lugha) kiengereza.(lakini mwanamke mwenyewe)

i hope i get it right:):lol:

Kenguy
February 11th, 2010, 04:33 PM
Salam Aleykum :D

I'd like to know how exactly is Swahili spread in Kenya and Tanzania like... does everyone use it??

And how good do people speak English or French? Especially educated people, I guess they all have a good command of these languages?

In Kenya and Tanzania, almost everyone speaks Swahili. Though in Kenya, English is widely used compared to Tanzania. Rwanda uses all three languages (English, French, Swahili) while Burundi use two (French, Swahili). Uganda uses more English than Swahili.

BUTEMBO21
February 11th, 2010, 04:46 PM
let me try to rewrite what butembo wrote in kenyan version.

mimi napenda vile waengereza wana sema (lugha) kiengereza.(lakini mwanamke mwenyewe)

i hope i get it right:):lol:

Right on target.:lol:

BUTEMBO21
February 28th, 2010, 11:47 AM
Sasa mu ishaka enda wapi?

Na ule mutu ya Ghana?

maasai1
February 28th, 2010, 02:11 PM
Sasa mu ishaka enda wapi?

Na ule mutu ya Ghana?

Ndugu Butembo, naamini unashangaa vile wahusika wa hii sehemu ya SSC hapa wamenyamaza sana. Pia yule ndugu mGhana hatuambii pale amefikia kwa jaribio lake la kujifunza kiswahili. Hata mimi sielewi vile wenzangu wamekuwa kimya hivi. Kiswahili kidumu!:cheers::cheers:

Kisumu Ndogo
March 1st, 2010, 01:23 AM

I thought he was from Uganda... Samahani. Nilidhania ni wa kutoka Uganda.

BUTEMBO21
March 14th, 2010, 05:03 AM
Ndugu Butembo, naamini unashangaa vile wahusika wa hii sehemu ya SSC hapa wamenyamaza sana. Pia yule ndugu mGhana hatuambii pale amefikia kwa jaribio lake la kujifunza kiswahili. Hata mimi sielewi vile wenzangu wamekuwa kimya hivi. Kiswahili kidumu!:cheers::cheers:

Si juwe kama baliisha endaka wapi, iko sa ule jamaa ya Ghana hana wakati, ju haku yake ata ku Oasis.

Kisumu Ndogo
October 19th, 2010, 07:31 AM
Burudika na Shairi: Na Ustadh Augustine J. Jeffrey (Mshairi)

http://reporter.leeds.ac.uk/526/pics/chiwara.jpg

Je, maisha yako timamu?

Sikulia lakini sasa nitalia

Tatu sasa ndizo siku

Usiku kucha usingizi sina

Ninayempenzi nimpendaye

Naye ywanipenda

Nina penzi langu

Mpenzi Nina uwapi?

uko huku Kenya

ama ulienda ulaya

au pengine nikazi Mombasa

Bila wewe moyo wangu siyo timamu

Kama malimau ni chungu

Nasikia uchungu moyoni

Sijui nitoroke niende nchi ya Mali,

nipigana na maisha

Vita kama vya Mau Mau

au nije Mombasa tule raha kisha tupendane

Maua nyekundu nitamnunulia nani?

Nina uwapi? Nina uchungu

Nasikia uchungu moyoni

Mayo! Nitawika kwa Kijaluo

Mayoye nitapiga kwa kijiji

Majirani ndio wao…na vijiti pamoja na mapanga

“Ndugu, je maisha yako timamu? Wataniuliza majirani

Wengi wao wakinywa chai ya majani

Kwenye vikombe vya rangi ya kijani

Kisumu Ndogo
October 19th, 2010, 07:51 AM
Lol

Zaitwa Lahaja. Nyie mwaongea lahaza ya Kingwana, Sisi wanairobi twaongea sheng ama Kimvita (Mombasa) au Kiamu (Lamu)

Kuna orodha ya lahaja mbali mbali kwenye kamusi elezi ya wikipedia

* Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.
* Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
* Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
* Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
* Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.
* Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
* Kingwana: Kiswahili cha Kongo
* Shikomor: Kiswahili cha Komoro
* Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
* Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
* Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
* Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba
* Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia
* Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya

Afadhali wakereketwa na mabingwa wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya wangelienzi lahaja za Kiswahili zilizochipuka Kenya; hususan lahaja ya Mvita au Amu kutumika mashuleni baadala ya ile iliyokubalika sasa ya Unguja labda Kiswahili cha Kenya hakingeathirika vile na Sheng maanake vyetu ni vitamu.

ernestombayo7
October 19th, 2010, 02:03 PM
Kuna mtu anaweza kunieleza ni vipi waganda (ugandans) wengine wanaweza kuzungumza Kiswahili? kwani kiswahili hufundishwa shuleni ama kuna enzi kiswahili ilifundishwa shuleni,wakati wa idi amin ama milton obote?

screenshotartist
October 19th, 2010, 02:52 PM
Kuna mtu anaweza kunieleza ni vipi waganda (ugandans) wengine wanaweza kuzungumza Kiswahili? kwani kiswahili hufundishwa shuleni ama kuna enzi kiswahili ilifundishwa shuleni,wakati wa idi amin ama milton obote?

Nilipokua Kampala siku waona Waganda wengi ambao wana ongea swahili.

Nilipo enda kwa miji na vijijini, Niliona kwamba wengi wana elewa swahili. Waganda hawafunzwi swahili shuleni, Lakini wengi wana jua na kujifunza kwa sababu ya maasiliano na waswahili majirani.

Waganda karibu na mpaka wa Congo wana ongea swahili kama ya Congo wale wakutoka karibu na mpaka wa Tanzania wana swahili kama ya TZ.

Kenguy
October 19th, 2010, 03:14 PM
Kuna mtu anaweza kunieleza ni vipi waganda (ugandans) wengine wanaweza kuzungumza Kiswahili? kwani kiswahili hufundishwa shuleni ama kuna enzi kiswahili ilifundishwa shuleni,wakati wa idi amin ama milton obote?

Waganda hawazungumzi Kiswahili sana kama watu wengine Afrika Mashariki. Wale ambao wanazungumza Kiswahili ni wanajeshi an watu ambao wanaishi karibu na mipaka ya Kenya, Tanzania na DRC. Pia katika jiji la Kampala na miji mikubwa nchini kuna watu wanaoweza kuongea Kiswahili.

Kiswahili hufundishwa shuleni kama lugha ya kigeni lakini wanataka kurekebisha hali hio na walazimishe ifundishwe kama vile wanavyofundisha Kiingereza.

Ernest, hujakosea kusema watu kama Idi Amin na Obote walieneza lugha ya Kiswahili. Wanajeshi katika serikali hizo za Amin na Obote walikuwa wanaongea Kiswahili sana walipokuwa wanaongea na wananchi wengine. Lakini hapo ndipo shida ilitokea kwa sababu waliwatesa wananchi wa kawaida wakitumia Kiswahili mpaka watu walichukua lugha hio kama lugha ya kuwanyanyasa watu. Kuna watu wengi ambao hawapendi kuongea Kiswahili hata kama wanajua. Kwa maoni yangu, wazee ndio wanaojua Kiswahili kuliko vijana katika maeneo ya mashambani.

Mashambani, watu huongea lugha zao za kikabila. Katikati ya nchi karibu na Kampala, watu huongea Luganda, ukienda magharibi watu huongea Runyankole/Rukiga na Kaskazini watu huongea lugha ambazo zinafanana na Kijaluo kama Acholi, Langi na kadhalika.

Ilibidi nijifundishe kuongea Luganda na Runyankole ili niweze kuongea na watu wengi Uganda. Lakini natamani siku moja hali hii itabadilika na wananchi wengi watajua Kiswahili.

ernestombayo7
October 20th, 2010, 01:12 AM

ahsante kwa jibu lako.Ume eleza vizuri sana.Ingekua bora sana kama nchi zote sa EAC zingeweka kiswahili kama lugha zao za kimataifa.Mazungumzo ingekuwa sana,na hata ingesaidia uchumi ya nchi zote kwa njia ya urahisi wa kufanya biashara.

Lakini na hofia kiswahili Kenya kwa sababu Kiswahili sanifui iko karibu kukufa.Wengi wetu tumesahau kiswahili sanifu.na mpaka tuchanganye na kiingereza ili tuweza kuwasiliana.

mwanamwiwa
October 20th, 2010, 07:18 AM
Burudika na Shairi: Na Ustadh Augustine J. Jeffrey (Mshairi)

http://reporter.leeds.ac.uk/526/pics/chiwara.jpg

Je, maisha yako timamu?

Sikulia lakini sasa nitalia

Tatu sasa ndizo siku

Usiku kucha usingizi sina

Ninayempenzi nimpendaye

Naye ywanipenda

Nina penzi langu

Mpenzi Nina uwapi?

uko huku Kenya

ama ulienda ulaya

au pengine nikazi Mombasa

Bila wewe moyo wangu siyo timamu

Kama malimau ni chungu

Nasikia uchungu moyoni

Sijui nitoroke niende nchi ya Mali,

nipigana na maisha

Vita kama vya Mau Mau

au nije Mombasa tule raha kisha tupendane

Maua nyekundu nitamnunulia nani?

Nina uwapi? Nina uchungu

Nasikia uchungu moyoni

Mayo! Nitawika kwa Kijaluo

Mayoye nitapiga kwa kijiji

Majirani ndio wao…na vijiti pamoja na mapanga

“Ndugu, je maisha yako timamu? Wataniuliza majirani

Wengi wao wakinywa chai ya majani

Kwenye vikombe vya rangi ya kijani

Asante Ndugu,hii shairi imeandikwa na bingwa lakini sijaelewa maana yake.Je,mnaweza kunieleza? :)

mwanamwiwa
October 20th, 2010, 07:24 AM
ahsante kwa jibu lako.Ume eleza vizuri sana.Ingekua bora sana kama nchi zote sa EAC zingeweka kiswahili kama lugha zao za kimataifa.Mazungumzo ingekuwa sana,na hata ingesaidia uchumi ya nchi zote kwa njia ya urahisi wa kufanya biashara.

Lakini na hofia kiswahili Kenya kwa sababu Kiswahili sanifui iko karibu kukufa.Wengi wetu tumesahau kiswahili sanifu.na mpaka tuchanganye na kiingereza ili tuweza kuwasiliana.

Hata mimi nikona hofu juu ya Kiswahili sanifu nchini Kenya.Kwa mfano,mimi sidhani ninaweza kuandika Insha ya karatasi moja leo!:bash: :ohno:

maasai1
October 20th, 2010, 04:14 PM
Hivi karibuni nilimzungumzia Boss yangu kazini kwa kiswahili na nilishtuka wakati aliponikemea na kuniamrisha nitumie kingereza!

Kenguy
October 20th, 2010, 05:04 PM
Hivi karibuni nilimzungumzia Boss yangu kazini kwa kiswahili na nilishtuka wakati aliponikemea na kuniamrisha nitumie kingereza!

Tulipitisha katiba mpya. Kiswahili inafaa kutumiwa katika ofisi kama Kingereza.
Lakini sioni watu wakibadilika. Tumezoea kutumia Kingereza katika mawasiliano yetu ndani ya ofisi mpaka kutumia Kiswahili ni shida. Naandika kwa Kiswahili lakini najipata nikifikiria kwanza na Kingereza. Ni mara ngapi umewahi andika barua pepe kutumia Kiswahili?

Kisumu Ndogo
October 26th, 2010, 06:45 PM
Asante Ndugu,hii shairi imeandikwa na bingwa lakini sijaelewa maana yake.Je,mnaweza kunieleza? :)

Mtenzi huyu Augustine kulingana na (ukurasa pepe) niliyonakili amebobea Katika utenzi wa shairi za kimapenzi. Kwa ufupi hapa haswa hatuelezewi sababu ya mhusika mkuu na mpenziwe kutokuwa pamoja lakini bilashaka mshairi analalama kwa uchungu na fedheha kutokuwa na mpenziwe na anahofia kuonekana kama mwehu na wanavijiji.

mwanamwiwa
October 26th, 2010, 07:03 PM
Mtenzi huyu Augustine kulingana na (ukurasa pepe) niliyonakili amebobea Katika utenzi wa shairi za kimapenzi. Kwa ufupi hapa haswa hatuelezewi sababu ya mhusika mkuu na mpenziwe kutokuwa pamoja lakini bilashaka mshairi analalama kwa uchungu na fedheha kutokuwa na mpenziwe na anahofia kuonekana kama mwehu na wanavijiji.

Asante.Ninafikiri nimeelewa.:)

xJamaax
December 19th, 2010, 12:02 AM
nimekaa sana bila kuzungumza kiswahili!Nakumbuka nilipoenda Kenya, watu walikuwa wanasema accent yangu imebadilika. Sijui kwanini accen hubadilika

BUTEMBO21
December 22nd, 2010, 01:10 AM
nimekaa sana bila kuzungumza kiswahili!Nakumbuka nilipoenda Kenya, watu walikuwa wanasema accent yangu imebadilika. Sijui kwanini accen hubadilika

Ju ulifanya siku mingi inche ya inchi , na uli kuwa na ikala mu inchi yenye aba semake Kiswahili.

xJamaax
December 26th, 2010, 08:35 PM
Ju ulifanya siku mingi inche ya inchi , na uli kuwa na ikala mu inchi yenye aba semake Kiswahili.

Ni ukweli!Nimekaa sana nje ndio maana!

xJamaax
December 26th, 2010, 08:39 PM
Asante.Ninafikiri nimeelewa.:)

Mbona ulikuwa wakasirika na mimi Oasis?kwani hutaki niseme kile ninachofikiria kuhusu Kenya?Wataka tu nisifu Kenya ilhali kuna pia mabaya yanayoletwa kutokana na Nchi za kigeni kuingilia mambo yetu!

Kisumu Ndogo
February 16th, 2011, 07:37 AM
Asante.Ninafikiri nimeelewa.:)

Shairi nyingine ndilo hili.

Utenzi wa : Samuel Mwenda (Taabu bin Tabu) © 2010.

MIMI SIO USTADH

Malenga wanochipuka, na waliochuchumaa,
Wale waliotukuka, na waliokukomaa,
Wale waliosifika, na waliokudumaa,
Mimi sio ustadhi, ni jina nimepachikwa.

Silione jina langu, kashtukia jamani,
Sione shairi langu, nafasi ukalihini,
Sione ujumbe wangu, ukadhani wafitini,
Mimi sio ustadhi, kutaniwa nataniwa.

Kumi na nne miaka, nikifundisha shuleni,
Bila kugura tabaka, nikikalia motoni,
Bila upeo kufika, naishia ukingoni,
Mimi sio ustadhi, kudanganya nadanganywa.

Mwongo mmoja unusu, natetea Kiswahili,
Kisema yananihusu, sijakutana na mali,
Hata kombe sijabusu, wala kupata medali,
Mimi sio ustadhi, limbukeni asokua.

Siku nyingi nikiimba, harusini shereheni,
Hakuna aliyenipamba, tunatengana jioni,
Ngozi zao wanaamba, kivuta kwao nafsini,
Mimi sio ustadhi, kutumiwa natumiwa.

Kama si Mungu muweza, nilipofika siwezi,
Wengi wananipuuza, ni bora nilimaizi,
Ningali ninajikaza, kuusarifu utunzi,
Mimi sio ustadhi, kujikaza najikaza.

http://alexsfunplace.com/ADF/coloringbook/images/Aladdin_-_Sultan.gif

Karama Antuamuo, Laare.
Nakili:http://tabubintabu.blogspot.com/

Pule
April 8th, 2011, 06:05 AM
Guys, apologies for posting in English but I don't know Shwahili but I got a question that I would like you to help me with.

There's a song, unfortunately I forgot both the artist and the name of that song, but it's sung by a lady with a guy being a supporting vocalist and it's probably one of Kenya's local type of music but I heard it on Channel O. On the chorus the lady goes something like "una manji" and she indicates money with her fingers. At the initial stages of the song the guy goes like "they say Kenyan man are not charming". If anyone of you knows it, please tell me what they mean by "una manji" or even correct me on the spelling.

I hope my question is in order. Thanks in advance.

Kisumu Ndogo
April 8th, 2011, 07:17 AM

Iam not aware of the song. But the phrase you mention 'Una Manji.' Manji could have originated from the Indian subcontinent(Pertaining to name|noun) perhaps you meant 'Maji' for Water or 'Manzi' for lady in Swahili and Sheng respectively.

------------------------------------------------------

Siifahamu hilo nyimbo. Walakini msemo ulilonakili "Una Manji"(Sheng) yaweza kuwa limetokana na jina la bara Hindi(Kimantiki kuumanisha Jina la mtu) ama pia yaweza kumaanisha maji au mwanamwali(Msichana - Mpenzi) kwa Kiswahili.

kiligoland
April 9th, 2011, 03:52 PM
kama kawa, hapa panapendeza, kiswahili cha mutu ya chuma si mchezo,:cheers:

screenshotartist
April 10th, 2011, 09:56 AM
kama kawa, hapa panapendeza, kiswahili cha mutu ya chuma si mchezo,:cheers:

:lol:

screenshotartist
April 10th, 2011, 10:01 AM
Guys, apologies for posting in English but I don't know Shwahili but I got a question that I would like you to help me with.

There's a song, unfortunately I forgot both the artist and the name of that song, but it's sung by a lady with a guy being a supporting vocalist and it's probably one of Kenya's local type of music but I heard it on Channel O. On the chorus the lady goes something like "una manji" and she indicates money with her fingers. At the initial stages of the song the guy goes like "they say Kenyan man are not charming". If anyone of you knows it, please tell me what they mean by "una manji" or even correct me on the spelling.

I hope my question is in order. Thanks in advance.

It is really hard to pin point your question, I can think of a few but do these names ring a bell on who the artist might have been:

Amani
Nameless
Nonini
Waire
Prezo

kiligoland
April 10th, 2011, 03:40 PM
Prezo is intense,:cheers:

Kisumu Ndogo
April 10th, 2011, 05:43 PM
kama kawa, hapa panapendeza, kiswahili cha mutu ya chuma si mchezo,:cheers:

Kwa kweli Kiswahili cha Congo DR(na Wakongomani humu) kinaelekea kuimarika lakini kimeathirika sana na Lugha butu ya Kilingala.

screenshotartist
April 11th, 2011, 05:00 AM
^^ Usi seme vile. Kiswahili yenye tuna semaka ai fananake na lingala ata kidogo.

Shiye batu ba swahili ba kongo tuko tofauti na Bangala

kiligoland
April 11th, 2011, 05:12 AM
^^ Usi seme vile. Kiswahili yenye tuna semaka ai fananake na lingala ata kidogo.

Shiye batu ba swahili ba kongo tuko tofauti na Bangala

usijali kaka, nimeelewa ulichosema, :cheers:

screenshotartist
April 11th, 2011, 05:34 AM
usijali kaka, nimeelewa ulichosema, :cheers:

Je? Unaweza kuya elewa maneno haya??

Muko na se aseme "Mutu ya chuma" amu wezi kumu sikia, alafu hi, yenye shiye tuna tetelaka mu BK. Tuko na ma terme zenye zina weza kuku drogues mu luga mpaka una zani aiko tena kiswashili.

EDIT: Bk is Bukavu, a city in South Kivu

kiligoland
April 11th, 2011, 08:28 AM
Je? Unaweza kuya elewa maneno yaha??

Muko na se aseme "Mutu ya chuma" amu wezi kumu sikia, alafu hi, yenye shiye tuna tetelaka mu BK. Tuko na ma terme zenye zina weza kuku drogues mu luga mpaka una zani aiko tena kiswashili.

EDIT: Bk is Bukavu, a city in South Kivu

MNASEMA MTU WA CHUMA, HAMWEZI KUMSIKIA(KUMWELEWA).HALAFU YEYE SISI TUNA..... (MWITA?) MBUKAVU. TUPO NA (TERM?) MANENO YANAWEZA KU...LUGHA MPAKA UNADHANI HAKIPO TENA KISWAHILI. AU (KISWAHILI HAKIPO TENA) haha, samahani sijaelewa vizuri, maneno mengine sijayaelewa:)

screenshotartist
April 11th, 2011, 11:52 AM
MNASEMA MTU WA CHUMA, HAMWEZI KUMSIKIA(KUMWELEWA).HALAFU YEYE SISI TUNA..... (MWITA?) MBUKAVU. TUPO NA (TERM?) MANENO YANAWEZA KU...LUGHA MPAKA UNADHANI HAKIPO TENA KISWAHILI. AU (KISWAHILI HAKIPO TENA) haha, samahani sijaelewa vizuri, maneno mengine sijayaelewa:)

Very good :okay:

Lakini bado ume kosa.

Nime sema

"Nyinyi mna sema eti "mtu wa chuma" hau mu elewi vizuri. Jee sasa hii swahili ambayo sisi watu wa BK tuna ongea?? sisi tuna zile neno ambazo zina weza kuku dhoofisha kwenye lugha la Swahili hadi una weza kufikiri lugha hii, sii tena Swahili"

kiligoland
April 11th, 2011, 12:30 PM
Very good :okay:

Lakini bado ume kosa.

Nime sema

"Nyinyi mna sema eti "mtu wa chuma" hau mu elewi vizuri. Jee sasa hii swahili ambayo sisi watu wa BK tuna ongea?? sisi tuna zile neno ambazo zina weza kuku dhoofisha kwenye lugha la Swahili hadi una weza kufikiri lugha hii, sii tena Swahili" hehe sasa nimeelewa vizuri

Kisumu Ndogo
April 12th, 2011, 03:40 AM
^^ Usi seme vile. Kiswahili yenye tuna semaka ai fananake na lingala ata kidogo. Shiye batu ba swahili ba kongo tuko tofauti na Bangala

Nilikuuwa ninamaanisha kuwa Kiswahili hicho kimezongwa kwa upande na lugha kubwa kama Kilingala na nitaongezea; Kikongo, Kitshiluba na Kingwana(Eastern DRC Swahili) n.k.

Kisumu Ndogo
April 19th, 2011, 05:23 AM
Att: Learn to speak swahili; Beginners guide.
http://www.pbs.org/wonders/Episodes/Epi2/2_cult1a.htm

brayo
May 24th, 2011, 06:01 AM
hey pule,

is this the song you are talking about?http://youtu.be/3Dw4aDJ_qJA

Pule
May 28th, 2011, 09:54 AM
hey pule,

is this the song you are talking about?http://youtu.be/3Dw4aDJ_qJA

That's the one buddy.

Pule
May 28th, 2011, 09:57 AM
It is really hard to pin point your question, I can think of a few but do these names ring a bell on who the artist might have been:

Amani
Nameless
Nonini
Waire
Prezo

She's the one...

Kenguy
May 28th, 2011, 11:52 AM
She's the one...

Nonini's a he. LOL

musir
May 28th, 2011, 03:35 PM
Nimerudi kutoka safari nchini Tanzania na kuna kitu kimoja nimegundua. Sisi Wakenya hatujui Swahili. Kweli Wabongo wanaipenda lugha.

Kama jana niliingia duka ili niweze kutuma barua pepe katika mtandao nilikuta wanatumia Google katika lugha ya Kiswahili. Kuhesabu pesa kwa Kiswahili kwangu ilikuwa ngumu kwa sababu walikuwa wananiambia bei ya bidhaa kwa Kiswahili halafu nilijikuta nikifikiria bei kwa kiingereza kabla ya kununua kitu chochote. Habari za saa tatu Tanzania wanasoma kutumia Kiswahili wakati mimi nimezoea kusikia Habari za Kiingereza saa hizo nikiwa nyumbani Kenya. Kile kilichonifurahisha sana ni vile Watanzania wanachukua kila mtu kuwa kama ndugu wao. Mtu akiniita na hanijui Uganda anasema gwe, Kenya ni wewe lakini Tanzania ni Ndugu... Nilifurahi sana!

Dar es salaam imeendelea sana. Si kama vile nilikuwa nimefikiria hapo mbeleni. Nitaziweka picha zile nilichukua katika uzi {if thats what you call a thread in Swahili} ya Dar es salaam nikipata wakati.

TZ, Hongera.

HA HA HAAAAAA! HIYO UZI (THREAD) IMENIBAMBA!

Pule
June 12th, 2011, 03:45 PM
Nonini's a he. LOL
oh...lol

tanzan
September 19th, 2011, 02:28 PM
Nimerudi kutoka safari nchini Tanzania na kuna kitu kimoja nimegundua. Sisi Wakenya hatujui Swahili. Kweli Wabongo wanaipenda lugha.

Kama jana niliingia duka ili niweze kutuma barua pepe katika mtandao nilikuta wanatumia Google katika lugha ya Kiswahili. Kuhesabu pesa kwa Kiswahili kwangu ilikuwa ngumu kwa sababu walikuwa wananiambia bei ya bidhaa kwa Kiswahili halafu nilijikuta nikifikiria bei kwa kiingereza kabla ya kununua kitu chochote. Habari za saa tatu Tanzania wanasoma kutumia Kiswahili wakati mimi nimezoea kusikia Habari za Kiingereza saa hizo nikiwa nyumbani Kenya. Kile kilichonifurahisha sana ni vile Watanzania wanachukua kila mtu kuwa kama ndugu wao. Mtu akiniita na hanijui Uganda anasema gwe, Kenya ni wewe lakini Tanzania ni Ndugu... Nilifurahi sana!

Dar es salaam imeendelea sana. Si kama vile nilikuwa nimefikiria hapo mbeleni. Nitaziweka picha zile nilichukua katika uzi {if thats what you call a thread in Swahili} ya Dar es salaam nikipata wakati.

TZ, Hongera.

Nashukuru sana kwamba ile uzi ya kwanini waTZ wana hisia za chuki dhidi ya waKenya imefungwa kwasababu haileti tija baina yetu.Hawa ama sisi humu ni viongozi wa kesho halafu humu humu mnapigana majembe???

Ni kweli Kenya iko mbele kiuchumi sababu zinazoeleweka lakini Tanzania ina nafasi kubwa zaidi na tayari inapiga hatua kufikia malengo yake.

Jumuiya yetu ni ya kujivunia.

Utani wa jadi msiichukulie too serious mkaleta dhana potofu.Tembea uone...tena ukiambiwa mtani ni kitu kizuri kujenga mahusiano zaidi katika mila zetu.

Nimesoma Kenya na Uganda boarding schools. Nilivokuwa Kenya, nikawa nataniwa sisi twapiga porojo tuu na kazi hakuna! Ni kweli sisi wajua kuongea na wapenda porojo...kama vile Brazil wanapenda Samba! Yaani ni utamaduni wetu...hata WaKenya ambao wapo hapa Bongo wanapenda huu utamaduni!

Kuhusu Kazi eti sisi wavivu...njooni mje kujionea wenyewe jinsi twajenga nchi yetu.Ndio bado tuna masafa marefu lakini vile vile Kenya nao pia.

Mbona mlikuja kwa kasi mno kwa Babu wa Loliondo? Leo hii jamaa mmoja anasema ndo the only medicine contribution Tanzania has made! Lakini si mlikuja kwa maelfu hadi viongozi wenu.Je! tuliwazibia?

Kwahiyo nasema msichukulie too serious!:cheers:

xJamaax
September 19th, 2011, 07:43 PM
"Swahili Spika Pahili"

They need to edit the heading.:lol:

But we understand he's a learner.

Mkenyasili
September 19th, 2011, 08:05 PM
Nashukuru sana kwamba ile uzi ya kwanini waTZ wana hisia za chuki dhidi ya waKenya imefungwa kwasababu haileti tija baina yetu.Hawa ama sisi humu ni viongozi wa kesho halafu humu humu mnapigana majembe???

Ni kweli Kenya iko mbele kiuchumi sababu zinazoeleweka lakini Tanzania ina nafasi kubwa zaidi na tayari inapiga hatua kufikia malengo yake.

Jumuiya yetu ni ya kujivunia.

Utani wa jadi msiichukulie too serious mkaleta dhana potofu.Tembea uone...tena ukiambiwa mtani ni kitu kizuri kujenga mahusiano zaidi katika mila zetu.

Nimesoma Kenya na Uganda boarding schools. Nilivokuwa Kenya, nikawa nataniwa sisi twapiga porojo tuu na kazi hakuna! Ni kweli sisi wajua kuongea na wapenda porojo...kama vile Brazil wanapenda Samba! Yaani ni utamaduni wetu...hata WaKenya ambao wapo hapa Bongo wanapenda huu utamaduni!

Kuhusu Kazi eti sisi wavivu...njooni mje kujionea wenyewe jinsi twajenga nchi yetu.Ndio bado tuna masafa marefu lakini vile vile Kenya nao pia.

Mbona mlikuja kwa kasi mno kwa Babu wa Loliondo? Leo hii jamaa mmoja anasema ndo the only medicine contribution Tanzania has made! Lakini si mlikuja kwa maelfu hadi viongozi wenu.Je! tuliwazibia?

Kwahiyo nasema msichukulie too serious!:cheers:
Je wataka vita iendelee au ikome? Hayo yaliisha ndungu yangu tusonge mbele tukiwa pamoja.

Kenguy
September 19th, 2011, 08:15 PM

Umesema ukweli mkuu! :)

kiligoland
September 20th, 2011, 05:30 AM
Je wataka vita iendelee au ikome? Hayo yaliisha ndungu yangu tusonge mbele tukiwa pamoja.

Du, mkuu bora tuishie hapahapa :lol: Hatutaki vita iendelee, au unasenaje, :lol: Kama vipi :cheers: mkuu,

mkuu tanzan na kenguy, nathamini sana busara zenu, mungu awabariki, na mungu ibariki africa:)

bantugbro
September 21st, 2011, 12:42 AM
Ok more Kiswahili class...

MWANAUME MTUMIA DAWA ZA UKIMWI AOTA MATITI

http://api.ning.com/files/OAtsN39tRu9TuwPxU1o5lvheLyOJU4Nw5ial7tZfVtQp-5fjR897GDJ4SqS1gNAugFWrjF9XrAg-NKDMp-8WkgtI0yWTVGe9/breast.jpg

BAADHI ya wanaume wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kurefusha maisha wamejikuta wakivimba matiti yao na kuwa makubwa kama ya wanawake.

Vilevile, wanawake wanaotumia dawa hizo wanalalamika kukutwa na matatizo kadhaa ikiwa ni pamoja na ulemavu.

Joseph Mkanda (43) amekumbana na tatizo la dawa hizo ikiwa ni pamoja na kuvimba matiti. Mwanzoni alihisi ni kutopata chakula bora, lakini akagundua kwamba ni aina za dawa anazotumia.

“Naona aibu sana kutoka nje ya nyumba yangu, kwani nimepata matiti kama mwanamke…. Naona watu wakiniona watanicheka,” anasema mwananchi huyo ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Mtwara.

“Nilipokwenda zahanati ya kijijini nikaambiwa hilo ni jambo la kawaida kwa watu walioathirika na Ukimwi, hivyo sijui la kufanya wala pa kwenda,” anasema Mkanda.

Mwanamke Salima Omar (36) mwenye watoto saba kutoka Mtwara anasema mwili wake umekumbwa na matatizo kibao tangu aanze kutumia dawa hizo. Mmoja wa watoto wake wa kike alifariki mwaka 2006 muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwake.

Hata hivyo, Salima ambaye ni mke wa Hassan, na ambaye mwili wake umejaa vipele, na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, anaamini hali hiyo inatokana na kutopata lishe bora.

“Madawa haya ni makali mno, usipokula vizuri ni lazima yataivuruga afya yako,” anasema na kuongeza kwamba kuna siku analazimika kuyatumia madawa hayo bila kula chochote hususan anapokuwa mgonjwa sana.

Mwanamke huyo anasema kuna wakati hayatumii madawa hayo kutokana na ukosefu wa fedha ya chakula, kwani mumewe ni fundi wa baiskeli na yeye (Salima) hupoteza fedha anazopata kwa kunywea pombe. Hali hiyo imemsababishia kuuza mbuzi wote wa familia yake ili kumudu maisha.

Kama zilivyo familia nyingi katika Wilaya ya Mtwara ambazo zinakabiliwa na upungufu wa chakula tangu mwaka 2007, Salima naye yuko katika mkumbo huo.

Vilevile, licha ya kuwa mwathirika, mwanamke huyo bado anaendelea kuzaa. Miezi mitatu iliyopita alizaa mapacha ambapo mmoja wao alifariki na mwingine hali yake ni mbaya.

Hata hivyo, wataalam wa tiba wamewashauri wanandoa hao kuacha kuzaa, jambo ambalo huenda wakakubaliana nalo.
Source:
http://www.globalpublishers.info/

xJamaax
September 21st, 2011, 01:15 AM
^^ :laugh:

Mkenyasili
September 21st, 2011, 05:12 AM

http://www.globalpublishers.info/ Eeeew!

Mkenyasili
September 21st, 2011, 05:17 AM
Du, mkuu bora tuishie hapahapa :lol: Hatutaki vita iendelee, au unasenaje, :lol: Kama vipi :cheers: mkuu,

mkuu tanzan na kenguy, nathamini sana busara zenu, mungu awabariki, na mungu ibariki africa:)
Naam ndugu yangu yetu tu ni kula, kunywa na kukaa kwa furaha na bashasha. :cheers:

Kenguy
September 21st, 2011, 10:10 PM
^^ :laugh:

Kama ingekuwa wewe ungecheka?

Anaweza kubadilisha ARV's na atafute 'regimen' tofauti.

bantugbro
September 22nd, 2011, 05:45 PM
Haya pateni habari za kidaku...

NI LULU TENA

http://api.ning.com/files/UhehNhORqGRUCqDJng-gvCP47cO0pr6k02qRufFx7LHrwXAFuJ9mWcYMNOLF8yCNAni4luZvzNoIPSYFqUvCIGjen1uygxEt/_MG_0715.JPG

KATIKA kudhihirisha kuwa amekatika mshipa wa aibu, staa kinda wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kwa mara nyingine anatengeneza kichwa cha habari, safari hii ikiwa ni kudendeka hadharani na mwanaume, Amani lina kitu kamili.

Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na paparazi wetu, lilijiri ndani ya viunga vya Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam, Septemba 18, mwaka huu kwenye ‘bethidei’ ya muigizaji mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

MPANGO MZIMA
Katika tukio hilo, kulikuwa na utaratibu wa kusoma kuponi yenye maelekezo mbalimbali kwa waalikwa.
Utaratibu ulikuwa hivi; Kama mmoja wa waalikwa alishindwa kufanya kile kilichoandikwa kwenye kuponi, alitakiwa kulipa faini ya shilingi 10,000.

Ratiba iliendelea kama ilivyopangwa lakini wengi walishindwa kuamini macho na masikio yao baada ya jina la Lulu kufikiwa kwani ilibidi wale wenye ustaarabu na heshima zao watazame pembeni kukwepa aibu ya msanii huyo.

LULU ATAKIWA ‘KUDENDEKA’
Kuponi ya Lulu ilimtaka atafute mtu anayempenda kisha ‘amkisi’ bila kujali kama ni mwanaume au mwanamke.

Wakati wengi waliamini Lulu angelipa shilingi 10,000 na kuachana na mpango wa kudendeka, msanii huyo ‘aliwasapraizi’ waalikwa wenzake kwa kumtafuta mwanaume na kula naye denda hadharani.

Awali, baada ya kusoma kuponi hiyo, Lulu kwa kujiamini, aliinua macho huku na kule, kisha akamchagua msanii mwenzake, Soud Ally ‘Akui’ kabla ya kusogea naye mbele na kuanza kudendeka.

Kabla hawajaanza ‘upuuzi’ huo, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Issa Twaha ‘Nteza’ aliwahesabia hadi tatu na kuwaacha wajinafasi.

Bila tone la nishai, Lulu alidendeka ‘laivu’ na jamaa huyo hadi wakadondoka chini ambapo baadhi ya watu walisikika wakisema: “Ama kweli Lulu anakoelekea sasa ni pabaya.”

LULU ACHEKELEA
Baada ya mshikemshike huo, wawili hao waliachiana, wakasimama huku Lulu aliyekuwa amevalia kipensi kifupi kilichoacha nje mapaja akibaki anachekelea.

Amani lilimfuata Lulu kutaka kujua kulikoni kufanya mambo hayo hadharani huku akijua fika yeye ni kioo cha jamii, alijibu: “Hii ni sehemu ya furaha, hata hivyo haiwahusu.”

LULU AMEKUWA SUGU?
Lulu mwenye miaka 18 amesharipotiwa na matukio lukuki ya aina hiyo ikiwemo kulewa tilalila na kufanya vitimbi visivyovumilika katika uso wa jamii.

KUTOKA AMANI
Lulu anapaswa kujirekebisha mara moja kwani ‘asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu’, kwa hiyo asisubiri kufundishwa na dunia kwa sababu anaweza kujuta maisha yake yote.

xJamaax
September 22nd, 2011, 07:58 PM
Kama ingekuwa wewe ungecheka?

Anaweza kubadilisha ARV's na atafute 'regimen' tofauti.
Maze si vizuri kucheka watu kama hawa kwasababu si wao wenyewe wametaka kuwa hivyo.:okay:

bantugbro
October 5th, 2011, 06:25 PM
Hapa mbona kimya sana siku hizi, labda tupate burudani kidogo...
8cgVBKtGb9M&NR=1

Mintali
October 5th, 2011, 07:33 PM
Nani ana video ya wimbo wa Bahati Bukuku wa Ukiinuliwa na Mungu?

chamoto
October 30th, 2011, 08:02 AM
Kile kilichonifurahisha sana ni vile Watanzania wanachukua kila mtu kuwa kama ndugu wao. Mtu akiniita na hanijui Uganda anasema gwe, Kenya ni wewe lakini Tanzania ni Ndugu... Nilifurahi sana!

Kweli hii ya "ndugu" huwa tunachukulia kawaida sana lakini hii hujidhihirisha hasa ukiwa nje ya Tanzania. Wengi wetu tunaishi kama ndugu bila ya kujali utaifa, udini wala ukabila wa mwingine.

BUTEMBO21
October 30th, 2011, 08:23 AM
Nani ana video ya wimbo wa Bahati Bukuku wa Ukiinuliwa na Mungu?

Muimbayi moya ivi wa bule-bule.

MARK_S
January 5th, 2012, 09:12 PM
Je wataka vita iendelee au ikome? Hayo yaliisha ndungu yangu tusonge mbele tukiwa pamoja.

....I normally dont get to kenyan threads, I did saw the closed thread "why kenyan hate Tanzania or otherwise..."

Je wataka vita iendelee au ikome? Hayo yaliisha ndungu yangu tusonge mbele tukiwa pamoja.

as the matter of fact, you can just begin it.....I will be waiting...:cheers:

MARK_S
January 5th, 2012, 09:16 PM
Du, mkuu bora tuishie hapahapa :lol: Hatutaki vita iendelee, au unasenaje, :lol: Kama vipi :cheers: mkuu,

mkuu tanzan na kenguy, nathamini sana busara zenu, mungu awabariki, na mungu ibariki africa:)

.....if we do not know one another, these issues are set to continue......coz the fellaz seem not to know us better.:)

Zoola
January 9th, 2012, 07:44 AM
I dont speak Swahili, I speak Arabic.

Kisumu Ndogo
January 20th, 2012, 06:30 AM
.....if we do not know one another, these issues are set to continue......coz the fellaz seem not to know us better.:)

Mark_S wewe ndiye kejeli butu humu SSC-East Africa.. mwanzo itose makasi yako ndipo uiano baina yetu iweze kukita mizizi la sivyo vita hivi vya panzi(neema ya kunguru) vitaendelea..

Kisumu Ndogo
January 20th, 2012, 06:32 AM
I dont speak Swahili, I speak Arabic.

Karibu (dada).^^

xJamaax
January 23rd, 2012, 03:32 AM
Unadhadni anaelewa?:lol:

xJamaax
January 25th, 2012, 10:26 PM
The mod should change the Swahili part of the title to a more grammatical correct one. Something like "Jamvi La Kiswahili" or "Jukwaa La Kiswahili" .

lady gaga
February 4th, 2012, 02:29 PM
Habari:wave:

xJamaax
February 4th, 2012, 10:30 PM
Mzuri sana!:cheers2:

lady gaga
February 5th, 2012, 06:17 PM
Thanks mr jamma

kiligoland
February 6th, 2012, 04:03 PM
Mzuri sana!:cheers2:

:lol: kama kawa mkuu jamaa :cheers:

kiligoland
February 6th, 2012, 04:04 PM
Thanks mr jamma

:lol:

lady gaga
February 6th, 2012, 07:56 PM
Why are you laughing :( ? Did i just emberresed my self big time ?

kiligoland
February 6th, 2012, 08:07 PM
Why are you laughing :( ? Did i just emberresed my self big time ?

I thought his name is JAMAA :)

lady gaga
February 6th, 2012, 08:17 PM
Oh sorry then jamaa

xJamaax
February 7th, 2012, 10:51 AM
No problem LG.

It's just a username and not my real name.Misspelling it is not a big deal.:lol: