Hello, hizo jet bridges ni international standards na zote unazoona hapo zina uwezo wa kuhudumia a380, zote! kwa nini? kwa sababu ni adjustable, hapo mbele kwenye tairi zake zinapanda na kushuka kufuatana na urefu wa ndege. Na vilevile a380 inaweza kutengwa sehemu nyingine kabisa kivyake bila jet bridge watu wakapelekwa kwa basi kisha kupanda ngazi za kawaida tu. Inafanywa hivyo viwanja vyote tu ambako airbus 380 inakwenda. Kwa nini? kwa sababu ya upana wa mabawa yake, ikiwekwa kati ya hizo jetbridges hapo, basi itabidi chain reaction jetbriges zote za jirani na a380 zisogezwe pembeni, ili ziweze kuhudumia ndege zingine salama, lakini nafasi kubwa inapotea na airports hazipendi kwa kuwa ndege zingine zitakuwa zinacheleweshwa kutua kwa sababu ya a380 moja au mbili, ndio maana kama ni kutumia jetbridges basi a380 inawekwa pembezoni kwenye bridges za mwisho au mwanzo. Tatizo la a380 kuja tanzania au nchi za kusini mwa dunia ni wateja tu! siyo viwanja kwa sana. hata ilipokuja kwa dharura bado iliweza kuhudumiwa, kwa hiyo kama wateja wangekuwepo ingekuja kama kawaida na kuhudumiwa either from the same spot as previously or wangetafuta sehemu muafaka. Nadhani imekusaidia