SkyscraperCity Forum banner
1 - 13 of 13 Posts

·
Registered
Joined
·
556 Posts
  • Kampuni ya Huduma za Meli (www.MSCL.go.tz) pia imeendelea kutoa huduma hizo katika maziwa makuu. Kampuni hii ilisafirisha abiria 178,812 ikilinganishwa na abiria 254,472 waliosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka 2013/2014. Hii ni pungufu kwa asilimia 30. Sababu za upungufu huo ni pamoja na kusimama kwa meli ya MV Victoria na MV Liemba kutoa huduma.

  • Kampuni imekamilisha matengenezo ya meli ya MV Serengeti ili iweze kutoa huduma za uchukuzi kati ya miji ya Mwanza na Bukoba katika kipindi ambapo meli ya MV Victoria inaendelea kufanyiwa matengenezo.


    Image credit: FrooiOhnesorg / Flickr.​

  • Wakati bajeti ya mwaka 2014/2015 inawasilishwa, Wizara ilitoa taarifa kuhusu uchelewaji wa kuanza kwa ujenzi wa meli mpya nne katika maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa kutokana na gharama zake kupanda kwa asilimia 163 ya gharama zilizokadiriwa awali. Mradi huu utakaogharimu US$ 74.9 milioni, unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Denmark. Ili kurahisisha utekelezaji, mradi huu sasa umegawanywa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa meli hizo itahusisha usanifu wa kina na ujenzi wa meli moja (1) mpya katika Ziwa Victoria, meli moja mpya katika Ziwa Tanganyika na ukarabati wa meli ya MV Umoja. Aidha, zabuni ya ujenzi wa meli hizo na ukarabati wa meli ya MV Umoja zimetangazwa Aprili, 2015.

  • Aidha, ili kuimarisha huduma za uchukuzi katika maziwa makuu, katika mwaka 2014/2015, Wizara iliahidi kuanza ujenzi wa meli moja kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA). Kazi ya ujenzi wa meli mpya kwa ajili ya kutoa huduma za uchukuzi wa abiria na mizigo katika Ziwa Nyasa ilianza Januari, 2015 na inatarajiwa kukamilika Desemba, 2015 :|

  • Aidha, kazi ya ukarabati wa meli ya MV Butiama ili kuwahudumia wananchi wa Visiwa vya Ukerewe inaendelea ambapo vipuri vya kuifanyia matengenezo meli hiyo vimeagizwa nje ya nchi.

  • Pamoja na kuitangaza meli ya MV Liemba kama urithi wa Taifa (National Heritage), Agosti, 2014 Serikali za Tanzania na Ujerumani zilisaini makubaliano ya kuifanyia ukaguzi meli ya MV Liemba. Ukaguzi huo uliokamilika Desemba, 2014 ulibaini kuwa meli hiyo bado ni imara kuweza kutoa huduma za uchukuzi endapo itafanyiwa ukarabati. Makubaliano hayo pia yalihusu kuifanyia ukarabati meli ya MV Liemba ili iendelee kutoa huduma. Ukarabati huo utagharamiwa kwa pamoja ambapo Serikali ya Ujerumani itachangia 50%, Serikali ya Tanzania 25% na sekta binafsi kutoka Ujerumani 25%. Kazi inayoendelea sasa ni kufanya utafiti wa kubaini gharama halisi zinazohitajika kwa ajili ya ukarabati :|

  • Kampuni inayomilikiwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China (SINOTASHIP) imeendelea kutoa huduma zake kwa kutumia meli kubwa moja yenye uwezo wa kubeba tani 57,000 kwa wakati mmoja. Katika mwaka 2014/2015, meli hii ilifanya safari 7 kama ilivyopangwa. Jumla ya tani 350,000 zilisafirishwa ikilinganishwa na tani 330,000 zilizosafirishwa katika mwaka 2013/2014 :|

  • SINOTASHIP itakodi meli moja ya mizigo (charter-in) kutoka Kampuni washirika ya China Ocean Shipping Company (COSCO) ya China ili kuongeza ufanisi wa Kampuni na kutafuta fedha ili kujenga meli ya mizigo na kukamilisha utafiti wa kununua meli ya kusafirisha gesi (LNG).
Source: MoT 2015/16 Budget Estimates http://www.mot.go.tz/images/uploads..._Uchukuzi_kwa_mwaka_wa_fedha_2015_-_2016_.pdf

Profile: SINOTASHIP

As initiated by Chinese late Premier Zhou Enlai and Tanzanian former President Julius K. Nyerere in 1960's, the two governments decided to establish the Chinese-Tanzanian Joint Shipping Company in the principle of friendly cooperation and mutual benefit.

As one of the earliest economic and trade cooperation projects between China and Tanzania, Sinotaship started operation in Jan. 1967. The company was registered in Tanzania and headquartered in Dar Es Salaam and has local branches in Beijing and Singapore.

Source: GoT http://www.tanzania.go.tz/home/pages/1584
 

·
Registered
Joined
·
556 Posts
1 - 13 of 13 Posts
This is an older thread, you may not receive a response, and could be reviving an old thread. Please consider creating a new thread.
Top